4 Septemba 2015 - 20:58
Julian Assange: Qatar, Uturuki na Saudi Arabia zilikubaliana na kuuangusha utawala wa Syria

Julian Paul Assange mwanzilishi wa tovuti ya whistleblower ametoa siri ya makubaliano yaliofanywa na nchi za Qatar, Uturuki na Saudi Arabia ya kuiangusha serikali ya Syria

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Assange alifichua siri hiyo katika televishen ya Urusi akisema kuwa makubaliano hayo yalipishwa na kusainiwa kwa siri mwaka 2012 na nchi hizo tatu (Qatar, Uturuki na Saudi Arabia) huku nchi za Magharibi kama vile Ufaransa, Uingereza na Marekani wakiunga mkuno makubaliano hayo.
Aidha alisema washirika wa Marekani katika nchi za mashariki ya kati walisaini makubaliano hayo kwaajili ya kukuza uhasama dhidi ya serikali ya Syria, kiasi kwamba serikali ya Saudi Arabia ili kuonyesha uhasama wake ilifikia hata ya kukiuka hata mapendekezo ya waanzilishi wa fikra hiyo ambayo ni serikali ya Marekani katika suala hilo.
Vithibitisho na mashiko ya kuwepo makubaliano hayo ni miungoni mwa nyaraka nyingi za maficho ambazo zimeonyesha uovo wa baadhi ya matifa na serikali za mashariki ya katika zinazo tafuta nguvu kibabe ikiwemo msimaizi wao mkuu (utawala Saudi Arabia).
Machafuko ya kisiasa ya Syria yameanza mwaka 2011 ambapo mpaka sasa yamesababisha vifo vya watu 230 elfu. Huku Serikali ya Marekani na washirika wake huvisaidia vikundi vilio na silaha vinavyopigana na majeshi ya serikali ya Syria

mwisho wa Habari/290